Giacinto Longhin


Uchangiaji katika miradi ya Wikimedia

Article Images

Giacinto Bonaventura Longhin (kwa jina la kitawa: Andrea di Campodarsego; 22 Novemba 186326 Juni 1936) alikuwa askofu wa Italia wa Kanisa Katoliki na mwanachama wa Shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini.

Giacinto Longhin

Papa Yohane Paulo II alimtangaza Mwenye heri tarehe 20 Oktoba 2002.

Maisha

hariri

Longhin alishika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya shirika lake baada ya kupadrishwa, kama vile kuwa mwalimu huko Udine na kuwa Mhudumu wa Kanda kwa shirika lake. Alikuwa na urafiki wa karibu na Giuseppe Melchiorre Sarto, Kardinali Patriarki wa Venice, ambaye mwaka 1903 alipata kuwa Papa Pius X (alitangazwa kuwa mtakatifu tarehe 29 Mei 1954). Papa Pius X alimteua rafiki yake Longhin kuwa askofu wa Treviso baada ya kiti hicho kuwa wazi.[1] Alihudumu kama Askofu wa Treviso kuanzia mwaka 1904 hadi kifo chake.[2][3]

Marejeo

hariri

  1. Steven Wood. "Bl. Andrea Giacinto Longhin". Iliwekwa mnamo 20 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Blessed Andrea Giacinto Longhin". Saints SQPN. 3 Machi 2010. Iliwekwa mnamo 7 Aprili 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Andre Hyacinth Longhin (1863-1936)". Holy See. Iliwekwa mnamo 20 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.